Sakata la kiungo mshambuliaji kutoka nchini Ghana Bernard Morrison na klabu ya Young Africans limeibuliwa upya na uongozi wa klabu hiyo kwa kulitaja Shirikisho la soka nchini TFF.

Morrison ambaye kwa sasa anaitumikia Simba SC ametajwa na uongozi wa Young Africans kufuatuia sakata lake la kuihama klabu hiyo kwa shinikizo la kutokua na mtakaba wa muda mrefu kama ilivyokua inadaiwa na waajiri wake wa zamani.

Leo mchana Makamu Mwenyekiti wa Young Africans Fredrick Mwakalebela amezungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa mpaka sasa hawajapata majibu yoyote kutoka TFF, kufuatia malalamiko yao kuhusu mkataba wa kiungo huyo na klabu ya Simba SC ambao ulidaiwa una mapungufu.

Mwakalebela aliibua hoja hiyo mwishoni mwa mwaka jana kwa kusema mchezaji huyo alisaini mkataba feki jambo ambalo limefumbiwa macho na TFF.

Pia amesema kuwa Morrison alitakiwa kulipa fedha kwa kwa Young Africans, lakini mpaka sasa imekuwa kimya tofauti na wao wanapofanya makosa na kupewa adhabu mara moja.

Mwakalebela amesema: “Mkataba feki wa mchezaji mpaka sasa imekuwa kimya, tunaomba tuitwe tuthibitishe, ukweli kuhusu suala hilo ila tunamaliza ligi hatujaitwa.”

“Kamati ilisema mchezaji anapaswa arudishe fedha kwenye Klabu ya Yanga, hadi leo hakuna suala hilo kuona linazungumzwa na hakuna majibu na hakuna suala linalozungumziwa.

“Hatujasskia TFF,(Shirikisho la Soka Tanzania) likisema kuwa mchezaji huyo amelipa ama kuna taarifa yoyote inayohusu malipo yake.

“Ila ikitokea sasa ni suala la Yanga limetokea muda huohuo adhabu inatolewa kwa wakati na utaskia tunaambiwa kwamba tunakatwa kwenye mapato ya getini”.

Ngorongoro Heroes mtegoni tena AFCON U20
'VISIT KIDIMBWI' yamponza Manara, atakiwa kuomba radhi