Saudi Arabia imepinga tuhuma kwamba mwandishi wa habari, Jamal Khashoggi aliamriwa kuuliwa na kikosi cha mauji ndani ya ubalozi wake mdogo wa Istanbul nchini Uturuki, na kusema kuwa tuhuma hizo hazina msingi.

Gazeti la Washington Post liripoti kuwa limepata sauti zilizorekodiwa ndani ya jengo zinazodaiwa kuthibitisha madai yao kwamba Khashoggi aliteswa na kuuawa katika ofisi ya ubalozi huo.

Aidha, Ujumbe wa Saudi Arabia uliwasili nchini Uturuki kwa mazungumzo, ambapo maafisa hao walikanusha taarifa hizo, wakati uhusiano wa nchi hizo unazidi kuwa tete.

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan ameitaka Saudi Arabia kutoa picha za CCTV kuthibitisha maelezo yake kwamba Khashoggi aliondoka kwenye ofisi hiyo ya ubalozi akiwa salama.

Hata hivyo, Khashoggi ambaye ni raia wa Saudi Arabia anayeishi nchini Marekani tangu Septemba 2017 alikuwa akihofia kukamatwa, kwa kukosoa baadhi ya sera ya mwanamfalme Mohammed bin Salman na uingiliaji wa Riyadh katika vita nchini Yemen.

 

 

 

Video: Dkt. Bashiru, Lowassa watoana jasho mdahalo wa Nyerere, Sababu za kutumbuliwa wakuu wa wilaya hadharani
Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Oktoba 13, 2018