Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira, amesema kuwa amekutana na Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na kumsikiliza dhidi ya tuhuma zilizotolewa na mfanyabiashara huyo kuwa amemuomba rushwa ya shilingi milioni 5, ambapo Mghwira amewataka viongozi wabadilike.

Mghwira amesema kuwa kumekuwepo na malalamiko mbalimbali ya wafanyabiashara dhidi ya watendaji tofauti tofauti wa serikali, kutoka katika idara mbalimbali hali inayoashiria ukwamishaji wa masuala ya biashara kwa nchi.

”Nimemsikiliza DC yeye kama yeye sasa itabidi tuwaite wote kwa vile wafanyabiashara wamelalamika hadharani na imebidi na sisi kamati ya usalama ya Mkoa tuwaite tuwasikilize ili watueleze kama kuna kero zingine tuzipunguze” amesema RC Mghwira.

Julai 22 katika mkutano wa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro na wafanyabiashara wa mkoa huo, mfanyabiashara huyo alidai kwamba DC Sabaya alimpa vitisho na kutaka ampe rushwa ya kiasi cha shilingi milioni 5. Baadaye Sabaya alizijibu shutuma hizo kwa kusema si kweli.

IGP Sirro afunguka kuhusu askari waliofariki kwa ajali Rufiji
Mbatia ampongeza Rais Magufuli, "Amefanya makubwa yenye uthubutu hata wengine hawawezi"