Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif  Sharif Hamad, amemwandikia barua Gavana wa Benki ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu ili achukue hatua za kulishughulikia sakata la fedha za ruzuku zinazodaiwa kukwapuliwa na CUF upande wa Mwenyekiti anaetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Maalim Seif ameandika barua hiyo yenye kumbukumbu namaba CUF/HQ/AKM/003/017/01 na nakala zingine kuzituma kwa mamlaka mbalimbali.

Katika barua hiyo kwa Profesa Ndulu, Maalim ameamabatanisha kumbukumbu ya miamala ya fedha ilivyofanyika, pia amesema kuwa chama hicho kinaendelea na taratibu za kukamilisha hatua za kisheria ili kuwafikisha mahakamani wahusika wote walioshiriki  katika kuchukua fedha hizo, akiwapo Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi.

Amesema kuwa, Mutungi atakuwa na kesi ya pili na atashtakiwa kutokana na madai ya kushirikiana na walalamikiwa wale wale wa kufungua akaunti mpya ili wapewe ruzuku.

Aidha, amesema Jaji Mutungi amefanya hivyo huku akifahamu fika kuwa kuna kesi ya msingi iliyopangwa kusikilizwa Februari 2, 2017 mbele ya Jaji Kihiyo.

“Gavana baada ya Muhtasari huo, kwa masikitiko makubwa leo nakuandikia barua hii kukujulisha kuwa njama za kuiba fedha za ruzuku  ya CUF Chama cha Wananchi zimefanikiwa  kwa kufanya muamala wa jumla ya shilingi 369,378,502.64 toka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kwenda akaunti namba 2072300456 ya NMB tawi la Temeke januari 5 mwaka huu,”amesema Maalim.

Hata hivyo, hivi karibuni CUF upande wa Maalim Seif ulilalamikia hatua iliyochukuliwa na Jaji Mutungi kuwapa CUF upande wa Profesa Lipumba zaidi ya shilingi milioni 360 za ruzuku

 

Mbowe kitanzini tena,apewa siku 14 kulipa deni linalomkabili
Rais Magufuli amrudisha Bungeni Anne Malecela