Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine ameanza taratibu za kulifikisha mahakamani gazeti la kila siku la Tanzania Daima ikiwa ni pamoja na wamiliki na wachapaji wake kwa kumhusisha na njama za upangaji matokeo ya michezo ya Ligi Daraja la Kwanza.

Mwesigwa ametoa msimamo huo leo baada ya gazeti hilo kuchapisha habari inayodai alikuwa miongoni mwa waliohudhuria kikao cha upangaji matokeo ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

“Nimeshtushwa na kusikitishwa sana na habari hiyo juu yangu ambayo ni ya kutunga, yenye nia mbaya isiyokuwa ukweli wowote, kwani sijawahi kukaa na watu wowote kupanga njama yoyote iliyo kinyume na maadili ya mchezo wa mpira wa miguu ” alisema Mwesigwa.

Gazeti la Tanzania Daima toleo nambari 4143 la leo tarehe 7 Aprili 2016 lilichapisha habari katika ukurasa wake wa 24 chini ya kichwa cha habari ” Vigogo TFF wajikaanga” likisema katika ibara ya 7 kuwa kwenye mazungumzo yaliyochukua zaidi ya dakika 10 yalihusisha pia Katibu Mkuu wa TFF, Mwesigwa.

Lowassa amkosoa Magufuli, adai hali mtaani inatisha
Manny Pacquiao Kupigana kwa Mara ya mwisho Marekani Wiki Hii