Kwa mara ya kwanza Shabiki wa klabu ya Simba Salama Zalhata Bint Jabir amefunguka kuhusu nafasi ya usemaji wa klabu hiyo, baada ya kuhusishwa na taarifa hizo kwa muda mrefu.

Salama amekua midomoni mwa Mashabiki na Wanachama wa klabu ya Simba wakimpendekeza kuwa Afisa Habari wa wa klabu hiyo, baada ya kuondoka kwa Haji Manara mwishoni mwa mwezi Julai.

Salama amesema Simba SC ni timu anayoipenda tangu zamani na anaipenda kutoka moyoni mwake, lakini hajawahi kuongea na viongozi wa klabu hiyo kuhusu nafasi ya kuwa Afisa habari.

Amesema kama itatokea uongozi utamtangaza kuwa Afisa Habari ataipokea nafasi hiyo na itakua heshima kubwa sana kwake.

“Simba ni timu yangu toka zamani ninaipenda kutoka moyoni, lakini sijawahi kuongea na viongozi wa Simba kuhusu nafasi ya kuwa afisa habari.”

“Nadhani kuna mtu aliamua kuanzisha hili, ikitokea nikapewa hii nafasi kwangu ni baraka. Ni baraka kubwa sana kwangu ikatokea nikawa katika club ninayoipenda katika nafasi ya Afisa habari.” amesema Salama Jabir.

Nafasi ya Afisa Habari ndani ya klabu ya Simba SC kwa sasa inashikw akwa muda na Ezekiel Kamwaga ambaye alitangazwa na uongozi saa chache baada ya kuondolewa kwa Haji Manara.

Kocha Gomes ashusha pumzi Simba SC
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 21, 2021