Mtangazaji maarufu, Salama Jabir ameeleza jinsi kazi ya kukosoa video za muziki nchini ilivyopelekea kukwaruzana na Mwana FA baada ya kuuchana muonekano wake kwenye moja kati ya video zake, alipokuwa mtangazaji wa Planet Bongo ya EATV.

Akifunguka kwenye The Playlist ya 100.5 Times FM, Salama ambaye ni mtu wa karibu wa wasanii ‘maswahiba’ AY na Mwana FA, alisema kuwa alikutana na wasanii hao wakiwa kwenye gari moja huku yeye akiwa kwenye gari lingine, ndipo alipoamua kuwasalimia kwa mbali lakini alikutana na kitu kisichokuwa cha kawaida.

Alisema kuwa alipaza sauti yake kwa shangwe kumsalimia AY aliyeitikia vizuri lakini hali ilikuwa tofauti kwa Mwana FA ambaye aliichunia salamu yake na kisha kuambiwa baadae sababu za mchuno huo.

“Nikamwambia Hamisi (Mwana FA) vipi?… akanichunia,” alisema Salama. “Sasa mimi nikashangaa huyu jamaa vipi! Baadae sasa nikaja nikaambiwa na Ambwene kwamba jamaa aliku-mind kwa sababu ulimsema video yake kwamba hakupiga pasi,” alifunguka.

Salama aliendelea kushikilia msimamo wake kuwa kweli ‘FA’ alikuwa hakupiga pasi kwenye video hiyo.

Salama Jabir na mtangazaji wa The Playlist ya Times Fm, Lil Ommy

Salama Jabir na mtangazaji wa The Playlist ya Times Fm, Lil Ommy

Alisema kuwa katika kipindi hicho cha ukosoaji wa video alikuwa anakutana na changamoto ya kukosana na wasanii lakini baadae walikuwa vizuri wote kwakuwa walielewa kile walicholenga kukifanya.

Hivi sasa Mwana FA ni mmoja kati ya maswahiba wa Salama na amekuwa akitoa video na nyimbo kubwa. Hivi karibuni ameachia ‘Asanteni Kwa Kuja’ iliyopikwa na Hermy B wa B Hitz. Video na audio zote zimefanya vizuri kwenye media.

Video: Majaliwa - Serikali italinda amani kwa gharama yoyote
Jeshi la Polisi kuwasaka wanaolibeza na kushabikia uhalifu mitandaoni