Mshambuliaji wa Lipuli FC Daruweshi Saliboko, amesema wakati huu ambapo ligi imesimama kwa tahadhari ya mlipuko wa virusi vya Corona, anautumia vema kujiweka sawa ili atimize malengo yake

Nyota huyo anaewika na vijuu wa Mkwawa Wanaparuhengo kutoka Iringa  amesema malengo yake ni kuisaidia timu imalize katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi kuu msimu huu wa 2019/20, pamoja na kumaliza ligi akiwa katika orodha ya wafungaji wenye mabao mengi.

Saliboko amesema, ni ngumu kwa timu au mchezaji kuwa mapumziko ya muda refu halafu akarudi katika kiwango kilekile, lakini kutokana na ugumu wa ligi msimu huu na wingi wa timu zitakazoshuka daraja anaamini kuwa watarudi na ari mpya zaidi ya ilivyokua kabla ya kusimama kwa ligi.

Mshambuliaji huyo ameongeza kuwa, moyo na akili yake amevielekeza kwenye klabu ya Lipuli FC, kwa kuamini akifanya hivyo atakua na azma ya kuhakikisha anatimiza malengo aliyojiwekea pindi ligi itakaporejea.

Ligi kuu soka Tanzania bara imesismama huku klabu ya Lipuli FC ikiwa kwenye nafasi ya 13 kwenye msimamo, kwa kufikisha alama 33 baada ya kushuka dimbani 29. Klabu hiyo imepoteza michezo 14, imeshinda 9 na kutoka sare michezo 6.

Simba SC wanaongoza msimamo wa ligi kuwa na alama 71, wakifuatiwa na Azam FC alama 54 baada ya wote kucheza michezo 28, wakati vigogo Young Africans ni wa tatu kwa alama 51 za michezo 27 na Namungo wa nne wakiwa na alama 50 za michezo 28.

Hali ni mbaya kwa Singida United inayoshika mkia kwa alama 15 za michezo 29, nyuma ya Mbao FC alama 22 michezo 28, Alliance FC alama 29, michezo 29, Mbeya City alama 30 michezo 29 na Ndanda FC alama 31 michezo 29.

Uhispania: Maiti za wazee waliokufa kwa Corona zakutwa kwenye makazi
Wanajeshi wa Chad zaidi ya 90 wauawa na Boko Haram