Beki na nahodha msaidizi wa kikosi cha Mtibwa Sugar, Salim Mbonde amesema kuwa hawatishiki na pengo la pointi kumi lilipo kati yao na timu ya Yanga SC katika msimamo wa ligi kuu zaidi watakaza nia yao katika mbio za ubingwa hadi siku ya mwisho ya msimu ili kujua hatma yao.

Mtibwa ilianza msimu kwa nguvu kiasi cha kuonekana kama wangeweza kutoa ushindani katika mbio za ubingwa msimu huu lakini mambo yamewageukia na sasa wako nafasi ya 4 wakiwa na pointi zao 33.

“Msimu huu mgumu, ushindani ni wa hali ya juu. Mzunguko wa pili umekuwa mgumu, lakini pointi 10 sio nyingi sana kwani hata wao nao hawashindi mechi zote kwahiyo tuna imani bado unaweza tukashinda mechi zetu nyingine na wao wakapoteza vile vile”, anasema mlinzi huyo wa timu ya Taifa  ya Tanzania ambaye amekwishacheza jumla ya michezo 17 kati ya 18 ya timu yake.

Baada ya sare ya kufungana 1-1 na Ndanda SC siku ya jana Jumapili katika uwanja wa Nangwanda, Mtwara mabingwa hao mara mbili wa zamani hawatakuwa na mechi wiki hii kwa kuwa waliopaswa kuwa wapinzani wao Yanga SC watakuwa katika michezo ya klabu bingwa Afrika.

Wataenda Songea kucheza na Majimaji FC, Februari 20. Mtibwa imefuzu pia 16 bora ya FA Cup, unadhani Mtibwa inaweza kuiwakilisha nchi katika michuano ya Afrika kwa kushinda moja ya mataji ya ligi kuu au FA?

“Uwezo huo tunao kwani na imani na timu yangu kwa maana ya wachezaji na walimu kwa ujumla, kwani hao wanaopata nafasi ya kuwakilisha taifa kila mara lakini hawafiki mbali kwahiyo mabadiliko muhimu. Mashabiki wa timu yetu wazidi kutusapoti ili tuzidi kufanya vizuri kwani supoti yao ni muhimu kwetu.”

Bondia Ibrahimu Maokola Ajifua Kumkabili Joseph Sinkala March 12
Simba Kukwea Kileleni Baada Ya Miaka 3