Meneja wa mwanamziki Nassib Abdul maarufu kama Diamond Platnumz, Sallam alizungumza kuhusiana na nyimbo mpya ambazo hivi karibuni Diamond anatarajia kuzifanya na kuwashirikisha wanamziki wakubwa Marekani ambao ni  Rick Ross na Rihanna.

Katika mahojiano yaliyofanyika kipindi cha Campus Vibes cha Times FM, Sallam alifafanua zaidi kuhusu hatua iliyofikiwa ya collabo hizo. Sallam alidai kuwa collabo na Rick Ross imeshakamilika, huku ile ya Rihanna ikiwa kwenye hatua ya mwisho baada ya  CV na historia ya Diamond  kuwa tayari imeshatumwa kwa uongozi wa Rihanna ili kufikiwa maamuzi ya mwisho.

 

Iwe Mvua, Iwe Jua David Alaba Kutua Real Madrid
Video: Wauza maua Dar walia hali ngumu, watoa ombi kwa Serikali