Meneja wa Diamond Platinumz, Sallam ameweka wazi vita yake ambayo inakuwa vita ya kundi la WCB dhidi ya mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji, Ruge Mutahaba.

Sallam ambaye awali aliandika ujumbe kwenye Instagram akimshambulia mtu aliyedai kuwa ana lengo la kumpoteza Diamond Platinumz kwenye tasnia ya muziki, jana alimuweka wazi kuwa ni Ruge.

Katika ujumbe ambao ulikuwa ukisubiriwa na watu kuona jina la aliyekuwa akimshambulia, Sallam ameweka picha ya Ruge na kudai kuwa ameamua kumsitiri kwakuwa mmiliki wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amemuomba msamaha.

“Kwa Heshima ya Joe Kusaga kukuombea msamaha kwa leo Bw Ruge Mutahaba naamua kukusitiri, ila ukiendelea kuyafanya ambayo unayafanya basi nitayaanika maovu yako yote unayoyafanya kwenye Industry ya muziki. WCB haina tatizo na media yoyote na wala haina tatizo na Clouds Media Group ila huyu Ruge Mutahaba ndio mwenye tatizo #TumekataaKuwaKaa,” ameandika.

Kiini cha ugonvi wao bado hakijawekwa wazi ingawa Sallam alianza kuwa mbogo kwenye mtandao baada ya watangazaji wa kipindi cha Shilawadu kueleza jinsi walivyoshambuliwa na mwanafamilia wa WCB, Moze Iyobo.

Ruge hajajibu chochote kuhusu mashambulizi yanayoelekezwa kwake na Sallam.

TANZIA: Tambwe Hiza afariki dunia
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Februari 8, 2018 | Maswali kwa Waziri Mkuu

Comments

comments