Meneja wa Diamond na lebo nzima ya WCB,  Sallam Sharaff afunguka kuhusu mapenzi aliyonayo kwenye wimbo wa Mac  Muga wa Alikiba licha ya utofauti unaosemakana upo kati ya Lebo yake na Alikiba

Sallam ambaye alitumia muda wake kuchat na kujibu maswali ya mashabiki wake kupitia akaunti yake ya istagram ambapo walipomuuliza wimbo gani wa Kiba anaupenda na kuukubali alijibu ‘Mac Muga’.

Pia alieleza kuwa nyimbo zote za WCB anazikubali kwani ndio biashara yake hivyo ni lazima ajikubali yeye, kazi yake na wasanii wake kwa kile wanachokifanya katika tasnia ya burudani kwani anaamini kinachofanyika katika lebo yake ni kuitendea haki tasnia ya burudani na hilo linaonekana wazi.

Kuhusiana na msanii nje ya lebo ya WCB, Sallam alitaja baadhi ya wasanii na nyimbo anazozikubali kutoka kwa wasanii hao, akiwemo Ben Pol na nyimbo yake ya ‘Moyo mashine’,

Sallam kwa upande mwingine alimtaja  Barnaba Classic miongoni mwa wasanii wake bora anaowakubali na kibao chake kinachofanya vizuri sana kwani ameweza kugusa namana ya maisha ya wakaka wengi ambao hujulikana kuwa penda penda, kibao cha Lover boy.

Alipata nafasi chache ya kufichua siri ambayo  ivi karibuni itawekwa wazi, ”Harmonize yupo njiani kutoka na rekodi mpya”, ‘hivyo mashabiki wake mkae mkao wa kula kumsubiria mnyamwezi Rajabu Ibrahimu’.

 

Video: Obama alivyopunga mkono wa kwaheri kumpisha Trump
UVCCM: bila CCM Tanzania isingekuwa na Demokrasia huru