Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Salum Kassim Ali, amesema kuwa mfumo wa tume hiyo unahitaji kuboreshwa ili kuondoa malalamiko ya wadau wa uchaguzi.

Ameysema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, amesema mfumo unaotumika kuwapata wajumbe wa tume hiyo ni mzuri, lakini bado una matatizo kutokana na kulalamikiwa na wadau wa uchaguzi.

“Mazungumzo yapo nje, yanazungumzwa mengi sana kuhusu tume ya uchaguzi,lakini huku ndani hakuna tatizo na tumekuwa tukikutana mara kwa mara na wajumbe wote wa tume hii na tumekuwa tukifanya mazungumzo na kuafikiana”amesema Ali.

Pamoja na Ali kusema kwamba ZEC hakuna mpasuko, lakini mwaka jana baada ya Jecha kutangaza kufuta matokeo ya uchaguzi wa Rais na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi  kwa madai kuwa uligubikwa na kasoro kadhaa, Wajumbe hao waligawanyika huku wa kutoka CUF wakidai kuwa hawakushirikishwa katika maamuzi hayo.

Video: Sakata la Watanzania Malawi laibua mapya, Makubwa yafichuka Faru John...
Lukuvi kula sahani moja na vigogo wanaomiliki majengo nchini