Mgombea Ubunge Jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salum Mwalimu amesema kuwa atakuwa mstari wa mbele kuhakikisha hakuna atakayevuruga matokeo.

Amesema kuwa amekuwa katika mfungo kwa siku zote za kampeni ili kuomba kupata ujasiri wa kutetea haki za wananchi wa jimbo la Kinondoni.

“Nawaapia Wallah,,,,Wallah,,,, nitakuwa wa kwanza kupigwa pingu na polisi kuliko kuona mtu yeyote akivuruga mchakato wa uchaguzi,”amesema Salum Mwalimu

Aidha, amesema kuwa baba yake alikuwa mwanajeshi na alifia vitani huku akiwaacha wakiwa watoto wadogo, hivyo haogopi kufa akitetea haki za wananchi wa Jimbo la Kinondoni.

Hata hivyo, ameongeza kuwa tangu kuanza kwa kampeni amefanya mikutano 21 ya hadhara na midogo zaidi ya 27, hivyo amesema hatokuliana na mtu yeyote atakayetaka kuvuruga uchaguzi huo.

Video: Chadema wapigwa, CCM mambo poa
Hali yazidi kuwa tete nchini Ethiopia