Salamu ya heshima ya kijeshi ‘Salute’ huenda ikawagharimu askari wa Jeshi la Polisi ambao watakutana na wabunge na kusahau ama kukataa kuwapa heshima hiyo.

Hayoyamewekwa wazi jana Bungeni baada ya Serikali kueleza kuwa askari wa Jeshi la Polisi ambao hawatawapigia salute wabunge watakabiliwa na adhabu za kijeshi ikiwa ni pamoja na kukatwa mishahara, kuondolewa kwenye kikosi kwa muda au kufaya usafi wa mazingira.

Hayo yalielezwa jana Naibu wa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha kwa alipokuwa akijibu swali kwaniaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Swali lililoulizwa na Mbunge wa viti maalum, Fakharia Shomari Khamisi wa CCM.

Aidha, Nasha aliwataka wabunge ambao hawatapigiwa salute na polisi kuripoti ili waweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Akitolea ufafanuzi suala hilo, Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Stella Mnyanya alisema kuwa agizo hilo linapaswa kwenda hadi kwa vyombo vya ulinzi vya makampuni binafsi.

Naibu Spika avunja rekodi, Aanza kujitetea Asing'olewe
vijana 20 wanufaika na ILO pamoja na NEEC