Samaki waliokuwa wamekamatwa na Waziri wa mifugo na Uvuvi, Luhanga Mpina wameanza kuuzwa leo mkoani  Mtwara.

Samakai hao walivuliwa kinyume cha sheria na Kanuni ya 66 ya Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu pamoja na kifungu cha 18 (2) cha Sheria ya Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya mwaka 1998 na marekebisho yake ya mwaka 2007.

Meli hiyo iliyohusika na uvuvi ni kutoka nchini Malaysia na kutozwa faini ya milioni 770 na kutakiwa kulipa fedha hizo ndani ya siku 7 kama namna ya kuadhibiwa.

Ilikamatwa Januari 26 mwaka huu baada ya kufanyika ukaguzi uliosimamiwa na kikosi maalum cha kupambana na kudhibiti uvuvi haramu na utoroshaji wa samaki na mazao yake wakati ikifanya shughuli za uvuvi katika ukanda wa Bahari Kuu kati ya Mkoa wa Lindi na Mtwara.

Endelea kufuatilia Dar24.com kuendelea kujua yaliyojiri ndani na nje Tanzania.

 

Maofisa EU wamtembelea Lissu
Haji Manara: Okwi anaendelea vizuri

Comments

comments