Kitendo cha nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta kufunga bao la kufutia machozi kwenye dimba la Anfield dhidi ya Liverpool katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kimemfanya aweke rekodi mbalimbali katika maisha yake ya soka na Tanzania kwa ujumla.

Samatta amesema goli alilofunga lilitokana na mpira wa kona uliopigwa vizuri na mchezaji mwenzake Bryan Heynen na kufanikiwa kusawazisha matokeo kwenye kipindi cha kwanza kabla ya kufungwa bao la pili katika kipindi cha mshambuliaji wa Liverpoll, Alex Oxlade Chamberlain.

”Namjua Bryan mara nyingi hunipasia na nafunga magoli mengi kutokana na ‘pass’ zake pia najua nikimbilie wapi ili niupate mpira atakaoupiga Bryan na nifunge goli na Ilikua kona nzuri yenye muunganiko mzuri hadi wavuni,” alisema Samatta.

Baada ya mchezo huo Samatta alisema chanzo cha kupoteza mchezo wa awali ilikua ni kucheza kwa kufunguka ili kuweza kupata matokeo katika uwanja wao wa nyumbani mbele ya mashabiki japo mambo yalikua tofauti pia amesema mchezo huo wa marudiano ulikua mgumu ambapo walitumia mfumo wa 5-3-2 lengo likiwa ni kuzuia mashambulizi ya wapinzani wao Liverpool.

”Nadhani mchezo wa nyumbani tulifungaki na kujaribu kutengeneza nafasi za mabao na kuonyesha mbele ya mashabiki wetu lakini mchezo huu wa leo tulikua na mabeki watano ambapo mara nyini tulikua tunazuia na hatukuhitaji kuwapa nafasi kwasababu tunajua wao wana ubora mzuri, washambuliaji wazuri na ushambuliaji mzuri kwahiyo tulijaribu kuwazuia,”alisema Samatta.

Samatta ameweka rekodi ya kuwa mtanzania wa kwanza kucheza michuano hiyo,mtanzania wa kwanza kufunga goli katika UEFA dhidi ya bingwa mtetezi, kufunga goli kunako Anfield, kuifunga timu inayoongoza msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza.

KRC Genk inayoshiriki ligi kuu nchini Ubeligiji ilicheza mchezo wa marudiano hivi karibuni dhidi ya Liverpool huku wakifngwa mabao 2-1 huku mchezo wa awali uliisha kwa Genk kukubali kipigo cha mabao 4-1.

Mwenyekiti auawa akitatua mgogoro wa Aridhi Kiteto
China yapika kasi ya 6G