Mabingwa mara tano wa kombe la dunia timu ya taifa ya Brazil, watacheza michezo ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Saudi Arabia na Argentina mwezi Oktoba.

Shirikisho la soka nchini Brazil (CBF) limethibitisha ratiba ya michezo hiyo ya kirafiki kupitia tovuti yake, baada ya kufikia makubaliano baina yao na viongozi wa mashirikisho ya soka ya nchi za Saudi Arabia na Argentina.

Brazil watacheza mjini Riyadh dhidi ya Saudi Arabia Oktoba 12, kisha watakutana na Argentina mjini Jeddah siku nne baadae.

Kikosi cha kocha Tite kwa mwezi huu kinakabiliwa na michezo ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Marekani na El Salvador.

Mchezo dhidi ya Marekani umepangwa kuchezwa mjini New Jersey leo Ijumaa na siku ya Jumanne watacheza dhidi ya El Salvador.

Video: Mbowe akimbiwa na wenyeviti 20 wa vijiji, "Acheni kumuenzi Nyerere kinafiki" JPM
Video: Mimi sikufukuzi mkurugenzi, chapa kazi- Rais Dkt. Magufuli

Comments

comments