Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemuwakilisha Rais Dkt. Magufuli katika Mkutano wa 37 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC ulioanza leo nchini Afrika Kusini, ambapo kesho pia anatarajia kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit).

Akizungumza mara baada ya kuwasili kwa Makamu wa Rais, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga amesema kuwa mkutano huo utapokea na kujadili ajenda mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa SADC na Uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Ushirikiano wa Siasa, Ulinzi na Usalama.

Amesema kuwa katika mkutano wa dharura wa wakuu wa nchi na Serikali wa Troika Mbili ya SADC (SADC Double Troika Summit)  Tanzania itakabidhi nafasi ya  Uenyekiti kwa Mwenyekiti mpya.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Double Troika inahusisha nchi wanachama sita ambao kwa sasa ni Swaziland, Tanzania, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Msumbiji, hivyo katika mkutano huo Mfalme Mswati III wa Swaziland atakuwa ndiye Mwenyekiti huku ajenda kuu katika mkutano huo ikiwa ni kupokea na kujadili taarifa kuhusu hali ya kisiasa, kiulinzi na kiusalama katika Kanda na hasa nchini DR Congo na Lesotho.

Jafo aamuru mkandarasi aliyetelekeza mradi wa maji asakwe
Mtatiro: Bora CCM kuliko kufanyakazi na Prof. Lipumba