Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bi. Samia Suluhu jana alifanya ziara katika mgodi wa dhahabu wa Geita (Geita Gold Mine) na kuelezwa kuhusu maendeleo ya uchimbaji na namna unavyowafaidisha wananchi.

Akiongea baada ya kuangalia uwasilishwaji (presentation), Bi. Suluhu alieleza kuridhishwa kidogo na mgawanyo wa kiwango cha fedha kwenda kwa watu lakini akaeleza kuwa bado amebaki na maswali kadhaa.

“Wakati naangalia presentation nimeona amount nzuri kidogo inatolewa kwenda kwa watu ingawa bado nina maswali yangu ambayo nitayafanyia kazi ili tuone ni kiasi gani sahihi kinatakiwa kutolewa na mgodi kwenda kwa wananchi, dhahabu iliyopo ni ya wana Geita Mungu amewaumbia katika ardhi yao,” Makamu wa rais alisema.

Bi. Samia alieleza kuwa wakati wa kampeni alipita katika mgodi huo na kusikitishwa na hali ya maisha ya wanachi wanaouzunguka mgodi huo. Alisema kuwa hivi sasa mgodi huo unapaswa kuwafaidisha moja kwa moja wananchi wa eneo hilo kwani wamebarikiwa kupewa madini ya dhahabu katika ardhi yao.

Hivyo, aliutaka uongozi wa mgodi huo kwa kushirikiana na viongozi wengine wa serikali kuhakikisha wanawezesha mgodi huo kuwafaidisha zaidi wananchi katika eneo hilo.

Utayapenda Majibu ya Mugabe kwa Mgombea urais wa Marekani aliyedai atamkamata na kumfunga jela
Mugabe awavuruga Manabii wanaomtabiria Kifo