Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani ameipongeza hospitali ya CCBRT kwa huduma bora wanazozitoa hususani za wagonjwa wa Fistula kwa wanawake kwa miaka 25 kwa kile alichodai kuwa wamefanikiwa wengi kurudisha heshima na utu wa heshima kwa wanawake wengi nchini.

Ameyasema hayo katika ziara yake kwenye hospitali ya CCRBT leo jijiji Dar Es Salaam baada ya kujionea huduma za afya ya Mama na Mtoto zilivyopiga hatua.

“Hakuna jambo kubwa Duniani kama kumrudishia mtu utu na heshima kwa wanawake waliokuwa wanatengwa na hata pengine kukimbiwa, kweli kazi mnayoifanya ni kazi ya Mungu,” amesema Samia Suluhu

Amesema kuwa huduma za Afya ya Mama na Mtoto kwa Mkoa wa Dar Es Salaam imefikia asilimia 80 ukilinganisha na miaka ya nyuma iliyopita, hivyo ameitaka Wizara ya Afya kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ili kupata takwimu zinazofanana kwenye utoaji wa huduma za afya nchi nzima.

Hata hivyo Mama Samia amesema kuwa licha ya Dar es Salaam kufikia asilimia hiyo ya huduma za Mama na Mtoto bado yanahitajika mafunzo ya kiutendaji na kitaalam kwa watoa huduma za afya ili kupiga hatua zaidi nchi nzima.

 

Magazeti ya Tanzania leo Juni 8, 2018
Mrema aanika uzushi uliotungwa na chama chake kuchafua Serikali