Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaagiza Majaji na Mahakimu wanawake kote nchini kupambana ipasavyo katika kukabiliana vitendo vya rushwa,unyanyasaji kijinsia na rushwa ya ngono ili kusaidia wanawake kupata haki zao za msingi bila kubaguliwa katika jamii.

 Ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa NANE wa Chama cha Majaji na Mahakimu wanawake Tanzania (TAWJA).
 Aidha,Samia Suluhu ametoa onyo kuhusu vitendo vya rushwa ya ngono inayofanywa na baadhi ya watendaji wenye madaraka na kusema tabia hiyo ni mbaya na lazima ikomeshw mara moja katika jamii.
Hata hivyo, amesema kuwa vitendo hivyo vya rushwa ya ngono huzuia na kukwamisha juhudi za wanawake kufikia huduma za kijamii na za kiserikali ipasavyo ikiwemo elimu, ajira na haki kwa ajili ya ustawi wa wanawake.
Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mohamed Chande Othman amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa mkakati wa uimarishaji wa shughuli za mahakama nchini unaendelea vyema lengo likiwa ni kutenda haki kwa wananchi kote nchini bila ubaguzi.
          

Maafisa uvuvi wazembe kukiona cha moto
Wolper na Harmonize wadaiwa kutafuta kiki