Katika kuhakikisha kuwa inakabiliana na ushindani uliopo sokoni na kwenda na wakati, Kampuni ya Simu ya Tanzania TTCL imezindua huduma mpya ya fedha mtandao ijulikanayo kama TTCL PESA ya Kampuni ya simu Tanzania TTCL.

Uzinduzi huo umefanywa mapema hii leo jijini Dar es saalam na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na kuhudhuriwa na Omari Nundu ambaye ni Mwenyeketi wa Bodi ya TTCL, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Anjelina Madete, Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Waziri Kindamba na wajumbe wa Bodi  na wafanyakazi wa TTCL.

Akizungumza katika hafla hiyo Makamu wa Rais amesema kuwa uzinduzi wa huduma ya TTCL PESA ni mwendelezo wa jitihada za Kampuni hiyo za kurejea katika nafasi yake ya awali ya kuwa suluhisho la kweli la utoaji huduma za Mawasiliano hapa nchini.

“Kuzinduliwa kwa huduma hii ni uthibitisho mwingine kwamba, TTCL inatekeleza kikamilifu maagizo ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais wetu mpendwa Dkt John Pombe Magufuli ambaye ameelekeza kuwa, Mashirika yote ya Umma yajiendeshe kwa faida, yatoe gawio Serikalini, yawahudumie wananchi kwa kiwango cha juu kabisa cha ubora na kwa gharama nafuu,”amesema Samia Suluhu.

Aidha, amesema kuwa TTCL PESA itawezesha wananchi kutuma na kutoa pesa kwa viwango vya chini kupita mitandao yote, pia itawezesha wananchi kulipia Bill za Umeme (LUKU), Maji, Ving’amuzi na kuwezesha wateja kununua muda wa maongezi na vifurushi vya data vya TTCL.

Hata hivyo, ameongeza kuwa TTCL PESA itatoa fursa kubwa ya ajira kwa wananchi kuwa mawakala na  itarahisisha shughuli za kiuchumi hasa biashara na hivyo aliwasihi wananchi kuonesha uzalendo wao kwa kutumia huduma za TTCL.

 

 

 

 

Video nyuma ya pazia 'Eneka' ya Diamond Platinumz
Wasanii bongo chukueni hii Kwa Beiber na Dj Khaled