Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Oktoba 11, 2016 amezindua mradi wa wodi ya wazazi  jijini Dar es salaam, uzinduzi huo umefanyika katika hospitali za Rufaa za Mwananyamala, Amana na hospitali ya Temeke, zilizopo halmashauri za manispaa za Kinondoni, Ilala na Temeke.

Samia Suluhu amewataka wafanyakazi wote kufanya kazi kwa bidii na kwamba kero zilizopo zinashughulikiwa na serikali, hivyo changamoto zinazojitokeza kwa sasa ni za muda mfupi tu baada ya muda zitamalizika, aidha amewapongeza wananchi wote kwa kujengewa jengo jipya na kuwaomba viongozi wa hospitali kumu unga mkono AMSONS ambao ndio wajenzi wa mradi huo pale watakapohitaji msaada.

”Changamoto ni nyingi tunaomba tuwaunge mkono viongozi wetu, tuwaunge mkono AMSONS waliojitokeza kutusaidia kutujengea wodi hizi kwa hospitali zetu tatu ,kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu nawaombeni tushikamane pale ambapo   changamoto ndogo ndogo zinapotokea kama upungufu wa  madawa,  gari la kubebea wagonjwa na upungufu wa majengo, serikali inayafanyia kazi yote.”  – Samia Suluhu.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Afya,  Khamis Kigwangala  amesema serikali kupitia wizara  hiyo wanafanya kila juhudi kupunguza vifo vya kina mama na watoto kwa kuhakikisha vifaa vyote wa huduma vinapatikana, aidha  amewashukuru na kuwapongeza wafanya kazi wa afya kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kuwaahidi  kuwapa ushirikiano wa karibu.

Hata hivyo kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewashukuru kampuni ya AMSONS Group kwa kujitolea kujenga wodi hizo za wazazi na kuwataka wadau wengine wenye nia ya kuleta maendeleo kujitokeza kwani  serikali ya awamu ya tano imetoa fursa kwa watu wote wenye nia njema ya kuleta  maendeleo.

Mradi huo wa ujenzi wa wodi za wazazi uko chini ya Amsons Group ambao mpaka kukamilika unatarajiwa kugharimu kiasi cha shil. bil. 4.5, na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi kumi na mbili.

 

 

Video: Makonda ataja mradi mwingine wa Bil. 8.8
Neil Warnock Amnusuru Marouane Chamakh