Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anatarajia kuzindua miradi mbalimbali mkoani Mara wakati wa ziara ya yake ya siku tatu mkoani humo.

Aidha, Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Mara imesema kuwa, Samia Suluhu atatembelea Wilaya ya Tarime, katika Kituo cha Afya cha Nyamwaga kinachojengwa na wananchi kwa msaada wa Mgodi wa Acacia North Mara.

Katika ziara hiyo  Samia ataweka jiwe la msingi katika Hospitali ya wilaya ya Serengeti kisha kuzungumza na wananchi mjini mugumu kwaajili ya kusikiliza kero mbalimbali wanazokumbana nazo.

Hata hivyo, mbali na kuweka jiwe la msingi, Samia Suluhu anatarajiwa kutembelea kiwanda cha Samaki cha Musoma Fish Processors kisha kuweka jiwe la msingi katika barabara ya km9.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami.

 

Video: Lissu afyatuka tena bungeni kuhusu mchanga wa dhahabu
Utafiti: Bodaboda, baiskeli hatari kwa nguvu za kiume