MAKAMU waRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amewataka Mawaziri wa Maji katika Nchi za Bara la Afrika kuhakikisha wanaweka mipango madhobuti itakayosaidia upatikanaji wa maji safi na salama kwa matumizi ya binadamu ili kunusuru idadi kubwa ya watu wanaopoteza maisha kila siku kutokana na magonjwa yanayohusiana na ukosefu wa maji safi na salama.

Mama Samia ameyasema hayo Jijini Dar es salaam alipokuwa akifunguwa Mkutano Mkuu wa wa kumi wa Baraza la Mawaziri wa Maji  wa Bara la Afrika-AMCOW-Mkutano ambao umehudhuriwa na Mawazi wa maji zaidi ya thelathini  kutoka Nchi za Afrika ambapo amesema takwimu zinaonyesha takribani watu mia nne wanapoteza maisha kila baada ya lisaa limoja kutokana na magonjwa yanayohusiana na ukosefu wa maji safi na salama hivyo amewataka mawaziri hao kuhakikisha  wanatumia mkutano huu kumaliza matatizo na changamoto za ukosefu wa maji katika Nchi za bara la Afrika.

Aidha amebainisha kuwa Ripoti kutoka Shirika la Afya Duniani-WHO-inaonyesha kuwa endapo mwanadamu atapata maji safi na salama kwa matumizi yake ya kila siku na kasha kuwa na mifumo bora ya uondoaji maji taka bila kuingiliana na maji ya matumizi ya matumizi yake atafanikiwa  kuepusha vifo vya watu milioni moja na laki nane ambavyo hutokea duniani kila mwaka, hivyo amesema kuwa maji yanamchango mkubwa katika kusababisha vifo au kunusuru maisha ya watu.

Akizungumzia upande wa Tanzania Makamu wa Rais amesema kuwa ili kuwezesha mpango wa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli wa kuwa na uchumi wa viwanda ni lazima kuwe na mifumo bora ya maji safi na maji taka kwa ajili ya matumizi ya viwanda bila kuleta madhara kwa binadamu.

Kwa upande wake Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Tanzania Mheshimiwa gerson Lwenge amesema malengo ya mkutano huu ni kuhakikisha maji yanapatikana kwa asilimia miamoja kwa Nchi za Afrika ifikapo mwaka 2030.

 

 

Zuio la Mikutano ya Kisiasa ni Kumnyima Mwananchi Uhuru wa Haki ya Kujumuika- Kijo Bisimba.
Mpango Wa Upimaji Wa Ardhi Dar Es Salaam Waja