Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa CCM Mkoa wa Kaskazini ‘A’  Unguja Zanzibar, kuwachukulia hatua wanachama wote wanao kisaliti na kukihujumu chama hicho.

Ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa mafunzo maalumu ya viongozi, watendaji wa CCM na jumuiya zake wapatao 556 ngazi ya Matawi, Kata, Tarafa na Majimbo katika Mkoa wa Kaskazini ‘A’ Unguja.

Aidha, amesema kuwa hatua hiyo itakisaidia chama kuimarisha shughuli zake, kuwa na wanachama waadilifu na wenye nia ya kuisaidia CCM kusonga mbele, kupata ushindi katika chaguzi zijazo.

“Ni muhimu kwa viongozi  wa chama kwenye ngazi zote washirikiane na viongozi wa Serikali katika maeneo yao ili kuhakikisha miradi ya maendeleo ya wananchi inafanyika kwa ubora unaotakiwa kulingana na thamani ya fedha,”amesema Samia Suluhu.

Hata hivyo, Makamu wa Rais amewaonya  baadhi ya wanachama ndani ya CCM akiwataka waache tabia ya kutengeneza makundi ndani ya chama ili wapate madaraka bali wawe mstari wa mbele kujenga umoja, mshikamano ndani ya chama.

TRA yawataka wafanyabiashara na wananchi kulipa kodi bila shuruti
Video: TFF yavunja mkataba na Mkwasa, yazungumzia michuano ya AFCON