Kiungo Samir Nasri amesema aliongezeka mwili kupita kiasi aliporejea Etihad Stadium wakati wa maandalizi ya msimu huu wa 2016/17.

Nasri amefichua siri hiyo alipohohojiwa na jarida la michezo la nchini Ufaransa (L’Equipe), ambapo amesema jambo hilo lilimlazimu kufanya mazoezi ya ziada katika kipindi cha maandalizi ya msimu kabla hajapelekwa kwa mkopo kwenye klabu ya Sevilla CF.

“Niliporejea Etihad Stadium kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi nilikua nimezidi uzito kwa kilo nne zaidi, hatu ambayo ilitoa msukumo kwa Pep Guardiola kunifanyisha mazoezi ya ziada ili nipungue na kufikia kilo 76,”

“Nilijaribu kufanya hivyo na hatimae nilipunguza kilo 2.5, na ndipo maamuzi ya kuruhusiwa kwa mkopo yalipofanyika.”

“Kiukweli kwa meneja kama Guardiola, amekua na mtazamo tofauti na mameneja wengine katika suala la kuzidisha uzito kwa mchezaji, inapofikia hatua unakua na uzito kwa zaidi ya kilo mbili na nusu, hautofanya mazoezi na wenzako na badala yake utapangiwa mazoezi yako binafsi.” Alisema Samir Nasri

Azam U-20 Kuanza Na Mbao Ligi Ya Vijana Kesho
Michael Carrick Asalim Amri Old Trafford