Kufuatia ripoti za matukio mengi ya watumiaji wa simu za Samsung kulipukiwa na simu hizo wakati wa kuchaji, kampuni hiyo ya Kikorea hatimaye imewataka watumiaje wake kutupa toleo la ‘Galaxy Note 7’ kutokana na tatizo hilo.

Kampuni ya Samsung imetoa tamko rasmi kupitia tovuti yake ikiwataka watumiaji wa simu hizo toleo la ‘Galaxy Note 7’ duniani kote kuchukua tahadhari na kuacha kabisa kuzitumia  wakati ikiendelea na uchunguzi zaidi.

“Tunafanya kazi na Mamlaka husika kufanya uchunguzi kuhusu kuwepo kwa ripoti za matukio yanayohusu Galaxy Note7. Kwa sabababu usalama wa mteja wetu ni kipaumbele, Samsung tunawataka wauzaji wote wa simu zetu duniani kuacha mara moja kuuza Galaxy Note 7,” imeeleza taarifa rasmi ya kampuni hiyo.

Majaribio ya betri ya simu ya Samsung, Galaxy Note 7 yaliyofanywa katika maabara moja nchini Singapore yalipelekea simu hiyo kulipuka moto.

Hivi karibuni, hata hapa Tanzania, kumekuwa na ripoti za matukio ya wananchi wengi kudai kuwa wameripukiwa na simu za Sumsung walipokuwa wanachaji. Pia, kulikuwa na taarifa ambazo hazikuthitishwa na Mamlaka kuhusu watu kulipukiwa na simu hizo walipozipokea wakati zikiwa kwenye chaji.

Hamisi Ali (sio jina halisi) aliiambia Dar24 kuwa yeye aliamka nyumbani kwake maeneo ya Kimara jijini Dar es Salaam na kukuta simu yake iliyokuwa kwenye chaji ikiwa imeunguza shuka na akafanya jitihada moto usishike godoro.

Mwanaume mmoja wa Kentucky, alisema kuwa yeye aliamka asubuhi na kuona simu yake ya Samsung, Galaxy Note 7 iliyokuwa kwenye chaji ikifuka moshi ndani ya chumba chake wakati akijiandaa kuwahi ndege, hivyo ilimbidi kutafuta namna ya kumaliza tatizo hilo la moto.

Serikali yakanusha kuwepo uhaba wa dawa muhimu
Ali Kiba aituhumu timu ya Diamond kwa ‘kumkanyagia waya’ show yake na Chris Brown