Nyota wa zamani wa Barcelona, Inter Milan na Chelsea Samuel Eto’o ameteuliwa kuwa kocha msaidizi  wa klabu ya Antalyaspor ya Uturuki.

Eto’o atasaidiana na kocha wa timu ya vijana ambaye pia ni mkurugenzi wa ufundi,  Mehmet Ugurlu.

Atapewa kazi hiyo kwa mkataba wa muda mrefu iwapo klabu hiyo itafanya vyema kwenye mechi tatu kabla ya mapumziko mafupi ya majira ya baridi.

Eto’o alijiunga na Antalyaspor kama mchezaji Juni 25 mwaka huu, kwa mkataba wa miaka mitatu na akawachezea mechi ya kwanza katika ligi hiyo Agosti 2015 dhidi ya Istanbul Basaksehir.

Alifunga mabao mawili mechi hiyo na kuwasaidia kushinda 3-2.

Eto’o, mwenye umri wa miaka 34 aliacha kuchezea timu ya taifa ya Cameroon mwaka jana.

Amepewa majukumu hayo mapya baada ya kufutwa kazi kwa kocha Simsek.

Hans Pope Atoa Ahadi Nzito Kwa Wanasimba
TP Mazembe Yaambulia Nafasi Ya Sita Duniani