Hatimaye Kamati Kuu ya CCM imetangaza majina ya makada watatu wa chama hicho waliopita katika hatua ya kwanza ya kinyang’anyiro cha kumpata mgombea wa nafasi ya Uspika wa Bunge la 11.

Kwa mujibu wa matokeo ya maamuzi ya Kamati Kuu yaliyosomwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, walioteuliwa ni Job Ndugai aliyekuwa naibu Spika wa Bunge la 10, Aballah Ali Mwinyi ambaye ni mtoto wa rais wa awamu ya pili na alikuwa waziri wa serikali ya awamu ya nne, pamoja na Ackson Mwansasu.

Kutokana na matokeo hayo, aliyekuwa Spika wa Bunge la 9, Samwel Sitta, Dkt Emmanuel Nchimbi na Mussa Azzan Zungu ni kati ya majina 20 yaliyokatwa.

Akielezea utaratibu unaofuata, Nape alisema kuwa majina hayo matatu yatapigiwa kura kesho na wajumbe wa chama hicho ili kupata jina moja litakalowasilishwa bungeni kwa ajili ya kupigiwa kura na wabunge wote.

 

 

 

 

Lowassa afunguka Kuhusu Msimamo Wa Ukawa Kuhusu Matokeo na Anachofanya Baada ya Kushindwa
Picha: Mjamzito Akining’inia Dirishani Kuwatoroka Magaidi Ufaransa