Baadhi ya wadau wa soka nchini Misri wametumia kurasa zao za mitandao ya kijamii kuonyesha kushangazwa na sanamu aliyotengenezewa staa wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah iliyojengwa nchini humo.

Salah ameungana na wachezaji walio na majina makubwa duniani, ambao wametengenezewa sanamu zao kutokana na kile walicho kifanya katika klabu zao na timu zao za taifa, miongoni mwa wachezaji walio tengenezewa sanamu ni Cristian Ronaldo na Lionel Messi.

Aidha, sanamu ya Salah imeonekana ikifananishwa na mtoto mdogo, haifanani na mtu mzima, hivyo baadhi ya wadau wamedai sanamu hiyo imetengenezwa kwa makosa na hakukuwa na sababu ya kufanya kosa hilo.

Hata hivyo, kuna wanao amini kuwa wajenzi wa sanamu hiyo waliishiwa na vifaa na ndio maana inaonekana kuwa na makosa tofauti na sanamu za wachezaji wengine, picha ya sanamu hiyo ya Salah inaonekana kuwa na muonekano wa mtoto wa miaka nane, hivyo imeonekana kama udhalilishaji.

 

Zawadi ya Khanga kwa wajawazito yapunguza vifo vya uzazi
Arsene Wenger anukia AC Milan

Comments

comments