Mchakato wa mshambuliaji kutoka nchini Chile Alexis Sanchez kuihama klabu ya Arsenal na kutua Manchester United upo mbioni kukamilika, kufuatia mchezaji huyo kuondolewa katika mazoezi ya kikosi cha kwanza.

Sanchez mapema hii leo aliwasili mazoezini kama kawaida lakini kutokana na mchakato wake kuwa njiani kukamilika, alilazimika kufanya mazoezi na wachezaji vijana ili kuendelea kujiweka fiti.

Mshambuliaji huyo hakujumuishwa na wenzake, kwa kuwa inahisiwa suala lake linaweza kuchangia kuondoa umakini mazoezini, katika kikosi cha kwanza ambacho mwishoni mwa juma hili kitakabiliwa na mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England.

Kikubwa ambacho kinasubiriwa katika uhamisho wa Sanchez, ni majibu ya kiungo mshambuliaji wa Man United, Henrikh Mkhitaryan ambaye anatajwa kuhusishwa katika dili hilo.

Lipuli yaifuata Mbeya City
Umoja wa Afrika wamuita Trump kikaoni, kumuweka ‘kitimoto’