Washika bunduki wa kaskazini mwa jijini London (Arsenal), watashuka dimbani siku ya jumamosi pasi na kiungo wao kutoka nchini Hispania Santi Cazorla.

Kiungo huyo ameshindwa kupita katika vipimo vya afya alivyofanyiwa, kufuatia jehara la kisigino linalomkabili tangu Oktoba 19, ambapo Arsenal walipambana na klabu bingwa nchini Bulgaria Ludogorets katika uwanja wa Emirates, na kuibuka na ushindi wa mabao sita kwa sifuri.

Cazorla amethibitisha kutokuwepo katika mchezo dhidi ya Man Utd, alipohojiwa na kituo cha radio cha Cadena COPE ambapo alisema mpaka sasa hajui ni lini atakuwa nje ya uwanja baada ya muda uliokua unatarajiwa kupita.

“Sijafahamu ni lini nitakua sawa kiafya, lakini jopo la madaktari linajitahidi ili kuniwezesha kurejea uwanjani haraka iwezekanavyo,”  Alisema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31.

The Three Lions Yamponza Adam Lallana
Hakimu awanyooshea kidole Polisi, Magereza kuhusu kesi ya Lema