Uongozi wa klabu ya Real Madrid umemtangaza Santiago Solari kuwa meneja kamili wa kikosi cha wakubwa hadi mwishoni mwa msimu wa 2020-2021.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 42, ametangazwa kushika wadhifa huo, baada ya kufaulu mtihani wa kukiongoza kwa kipindi cha majuma mawili kikosi cha Real Madrid, kufuatia kutimuliwa kwa aliyekua mkuu wa benchi la ufundi Julen Lopetegui.

Ushindi uliopatikana katika michezo minne tangu alipotangazwa kuwa meneja wa muda dhidi ya Melilla (Kombe la Mfalme), Viktoria Plzen (ligi ya mabingwa barani Ulaya), Real Valladolid na Celta Vigo (La Liga) umekua chagizo kwa Solari kutangazwa kupandishwa cheo na kuwa meneja mkuu.

Hata hivyo maamuzi ya uongozi Real Madrid kumtangaza Solari kuwa meneja mkuu, yametokana na Sheria za soka nchini Hispania, ambazo hazitoi nafasi kwa klabu yoyote kuwa na meneja wa muda kwa zaidi ya siku 15.

Kimahesabu muda wa Solari kuwa meneja wa muda wa Real Madrid ulifikia tamati tangu siku ya jumatatu juma hili, hivyo kulikua na ulazima kwa Real Madrid kumtangaza kuwa meneja mkuu, ama dili hili lingeenda kwa mtu mwingine.

Kabla ya kupandishwa na kuwa meneja wa muda wa kikosi cha kwanza, Solari alikua kocha wa timu ya vijana ya klabu hiyo tangu mwaka 2016, na alipewa nafasi ya kuwa kwenye benchi la ufundi la Real Madrid, baada ya kisago cha mabao matano kwa moja walichokipokea kutoka kwa FC Barcelona mwishoni mwa mwezi uliopita.

LIVE Bungeni Jijini Dodoma mkutano wa 13 kikao cha 7- Maswali na Majibu
Video: Siri ya Rostam kuteta na JPM, Fagio la Magufuli lamtisha waziri