Thamani ya penzi la Harmonize ndani ya moyo wa Sarah huenda inashabihiana na thamani ya madini ya Tanzanite kwake, na huenda ndio sababu mrembo huyu ameamua kujenga ‘ukuta’ kuhakikisha ulinzi dhidi ya wanaotaka kudokoa mali yake.

Hatua hii inathibitishwa na alichokifanya mrembo huyo mapema jana kwa kuweka wazi ujumbe binafsi wa Jackline Wolper kwa Harmonize, aliomtumia kupitia ‘inbox’ ya Instagram akieleza jinsi ambavyo bado moyo wake unalikumbuka penzi la mkali huyo wa WCB na kujuta.

Katika ujumbe huo ambao Sarah aliuweka kwenye akaunti yake ya Instagram, Wolper amemchokoza tena Harmonize kwa kumtumia video inayowaonesha wakiwa pamoja na kuandika, “zinaniuma sana na najuta kupita kiasi. Nablock kila anayepost.”

Sarah ameweka picha hizo na kuandika, “desperate girl u dm my baby yesterday @harmonize_tz and you speak alone. Live u life baby @wolperstylish.” Kwa tafsiri isiyo rasmi amemuita Wolper kuwa ni msichana anayetapatapa na kwamba alimtumia ujumbe mpenzi wake lakini akajikuta anaongea mwenyewe. Amemtaka aishi maisha yake huku akimkejeli.

Hata hivyo, Wolper alishindwa kunyamaza na kujibu mashambulizi kwa kuweka video maarufu ya Nicki Minaj akicheka na kuandika, “#confidenceisthebestoutfitrockitandownit”, akimaanisha kujiamini ni vazi bora zaidi, livae na ulimiliki.

#selfconfidenceisthebestoutfitrockitandownit👌

A post shared by @ wolperstylish on

Wolper alikuwa mpenzi wa Harmonize kwa muda lakini nafasi yake ilichukuliwa na Sarah ambaye anaonekana kulipa uzito unaotakiwa penzi la mwimbaji huyo. Hivi karibuni, walikuwa na mama yake Harmonize wakifanya utalii wa ndani kwenye hifadhi ya taifa.

Ukuta wa Sarah unaomzunguka Harmonize ni wa aina yake, hili linaweza kuwa ni onyo kwa wasichana wengine wanaotaka kumdokoa kuwa jumbe wanazotuma ziko kwenye hatari kubwa ya kusomwa na mrembo huyo.

 

Msafara wa Mayweather washambuliwa kwa risasi.
Spika ajiuzulu kukwepa kura ya kung'olewa

Comments

comments