Mshambuliaji wa zamani wa Rayon Sports Michael Sarpong amekiri ni kweli kuna mazungumzo yamefanyika kati ya wakala wake na uongozi wa Young Africans, lakini bado hajafanya maamuzi.

Hivi karibuni kocha Mkuu wa Young Africans Luc Eymael alifichua kuwa Sarpong ni miongoni mwa wachezaji anaowahitaji kwenye kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao.

Nyota huyo raia wa Ghana mwenye umri wa miaka 23, amesema amepokea ofa kutoka timu nyingi, hivyo anahitaji muda ili afanye tathmini kabla ya kuamua.

“Ni kweli, Yanga walinikaribia tukazungumza lakina sijachakua uamuzi. Nina ofa nyingi, napaswa kwanza nitulie tutafanya mambo kwa utulivu. Wakala wangu atamaliza kazi,” amesema

Sarpong mkataba wake ulivunjwa na Rayon Sports mwezi uliopita baada ya kuingia kwenye mtafaruku na viongozi wa timu hiyo.

Hata hivyo alikuwa mwishoni mwa makataba wake wa miaka miwili ambao ulikuwa umalizike mwishoni mwa msimu.

Sarpong aliifungia Rayon mabao 24 katika misimu miwili aliyoitumikia klabu hiyo ya jijini Kigali.

Watanzania 23, madereva wakutwa na Corona mpaka wa Namanga
Ajibu ataja sababu zilizomuengua kikosini