Kamanda wa kikosi cha polisi usalama barabarani, Fortunatus Musilimu amesema kuanza sasa kikosi hiko kimeanzisha oparesheni kabambe ya kuhakiki leseni za madereva kwa njia ya kielektroniki ambapo kutakuwa na fomu maalumu na kila dereva atahakikiwa kwa kujaza taarifa zake muhimu.

Amesema pamoja nakuwa ukaguzi wa leseni unaendelea wataanza kukagua leseni za madereva wa magari ya kubeba abiria, madereva wa  magari ya kubeba mizigo, madereva wa pikipiki na kumalizia kwa madereva binafsi na magari ya serikali.

Ambapo utaratibu utukaotumika kuhakiki leseni hizo ni pamoja na fomu maalumu ambazo zitajazwa zitakazorahisisha kumtambua dereva ambaye leseni yake imehakikiwa na yule ambaye bado leseni yake haijahakikiwa.

Fomu hiyo itabeba taarifa za dereva mwenyewe, darala la leseni yake, na tarifa za shule au chuo alikosomea udereva lakini pia fomu hiyo itasainiwa na dereva mwenye pamoja na askari aliyefanya uhakiki huo.

Kamanda Musilimu ametoa tahadhari kwa dereva atakayetoa taarifa zake ambazo siyo sahihi kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake pamoja na askari aliyemfanyia uhakiki.

Amesema lengo kubwa la oparesheni hiyo ni kuwa na madereva makini na mahiri amabao watasaidia kuhakikisha ajali za barabarani zinazotokana na uzembe wa madereva zinatoweka.

Aidha amemalizia kwa kusema Kuwa ukaguzi wa leseni za madereva wa magari makubwa utafanyika maeneo ya mizani na standi za mabasi, ila madereva wa magari binafsi ukaguzi utaendelea kufanyika barabarani na vijiwe vya waendesha pikipiki lengo ni kuhakikisha leseni zote nchini zinakaguliwa.

Video: Yanga yafanya uteuzi mrithi wa Clement Sanga
Kesho Waziri Mkuu kuongoza zoezi la usafi Coco beach