Uongozi wa Chelsea ukiongozwa na mmiliki wa klabu hiyo bilionea Roman Abramovich umemfungashia virago kocha mwenye utajiri wa maneno,  Jose Mourinho.

Klabu hiyo imefikia uamuzi huo kutokana na kuporomoka kwa timu hiyo kubwa duniani na kumruhusu kichapo kisichotarajiwa hata katika Uwanja wa nyumbani.

Klabu hiyo imempa nafasi Guus Hiddink kuinoa timu hiyo kwa kipindi kilichobakia katika msimu huu.

Mourinho ambaye alikuwa mmoja kati ya makocha bora zaidi duniani anakuwa meneja wa nane kutimuliwa na mmiliki wa Chelsea tangu mwaka 2003.

Kocha huto aliwahi kujitabiria Maisha marefu katika klabu hiyo akijitaja kama mtu Muhimu na kocha bora anaezidi kufanya vizuri kila kukicha. Ndoto yake hiyo ndani ya Chelsea imezimwa rasmi leo.

 

Mnyika hajaridhishwa na hatua zilizochukuliwa na Waziri wa Maji, Aomba Waziri Mkuu Aingilie Kati
Ben Pol ampa 'makavu' Ali Kiba