Hatimae Wales imefanikiwa kupanda katika viwango vya ubora wa soka duniani ambavyo vimetolewa muda mchache uliopita na shirikisho la soka duniani FIFA na kuwapita ndugu zao England.

Mafanikio ya kutinga kwenye hatua ya nusu fainali ya Euro 2016, yamekua chachu kwa nchi hiyo kupanda katika viwango hivyo na kufikia nafasi ya 11 tofauti na England wanaokamata nafasi ya 13.

Nahodha na mshambuliaji wa pembeni, Gareth Bale pamoja na wenzake walikua gumzo wakati na baada fainali za Euro 2016 hali ambayo imedhihirisha walijiandaa kufikia malengo, hasa pale walipoichakaza Ubelgiji mabao matatu kwa moja na kutinga katika hatua ya nusu fainali.

Mbali na kuwa juu ya England, pia Wales inakamata nafasi ya kwanza katika nchi ambazo zipo chini ya utawala wa Malkia (Great Britain).

Kocha Chris Coleman amekua chagizo la mafanikio hayo, baada ya kuipandisha Wales kwa nafasi 15 kutoka nafasi ya 26 ambayo walikua wakiikamata kabla ya fainali za Euro 2016 kuanza Juni 10 na kumalizika Julai 10.

Ifuatayo ni orodha ya 20 bora katika viwango vya ubora wa soka duniani ambavyo vimetolewa na FIFA muda mcheche uliopita.

1        Argentina

2        Ubelgiji

3        Colombia

4        Ujerumani

5        Chile

6        Ureno

7        Ufaransa

8        Hispania

9        Brazil

10      Italia

11      Wales

12      Uruguay

13      England

14      Mexico

15      Croatia

16      Poland

17      Ecuador

18      Uswiz

19      Uturuki

20      Hungary

Waziri Mkuu Apokea Msaada wa Madawati 500 Kutoka China
Majaliwa akagua Ujenzi wa Kiwanda cha Vigae (Tiles)