Klabu ya Borussia Dortmund ya nchini Ujerumani, imekanusha taarifa za kuanza mazungumzo na uongozi wa Manchester City kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji kutoka Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang.

Afisa habari wa klabu hiyo ya kaskazini mwa Rhine-Westphalia, Sascha Fligge amesema hakuna mazungumzo yoyote yanayoendelea ya usajili wa mshambuliaji huyo, na amewataka mashabiki wa soka duniani kote kupuuza habari hizo.

Fligge amesema wamekua wakiona taarifa hizo katika mitandao ya kijamii pamoja na tovuti za michezo lakini hawafahamu lolote kuhusu mazungumzo ambayo yanaripotiwa kuanza tangu juzi.

“Hatujui lolote kuhusu mazungumzo hayo,”

“Tunashangazwa na taarifa hizo na hatufahamu zimetokea wapi mpaka kufikia hatua ya kuwekwa katika mitandao ya habari na ile ya kijamii duniani kote, ninaomba zipuuzwe.” Amesema Sascha Fligge

Sascha Fligge

Man City wameripotiwa kuwa katika mazungumzo ya usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26, na wameonyesha kuwa tayari kutoa kiasi cha Pauni milion 50.

Aubameyang ameonekana kuwa tegemeo kubwa la, Dortmund na kwa msimu uliopita alifanikiwa kufunga maboa 39.

Liverpool Wahangaika Na Usajili Wa Mshambuliaji
Brazil Yakumbuka Kichapo Cha Kufungwa Mabao Saba

Comments

comments