Nchi ya Saudi Arabia imeamua kuruhusu ujenzi wa makanisa baada ya kusainiwa kwa makubaliano kati ya viongozi wa Wahhabi na Kadinali wa Vatican.

Makubaliano hayo kati ya Rais wa Baraza la kipontifiki ya midahalo ya dini mbalimbali, kadinali Jean Louis Tauran na Sheikh Mohammed bin Abdel Karim Al-Issa ambaye ni katibu Mkuu wa NGO kubwa ya Wahhabi yanalenga kuruhusu ujenzi wa makanisa pamoja na mikutano ya Waislamu na wakaristo mara moja kila baada ya miaka miwili.

Saudia Arabia ni moja ya nchi zisizo na uvumilivu kwa dini nyingine zaidi ya uislamu. Wasio waislamu wanaadhibiwa kwa kuonesha matendo ya dini yao nje ya nyumba zao huku Muislamu yeyote anayeamua kubadili dini kuhukumiwa kifo. Sheria za kiislamu zinawahusu wote wanaoishi nchini humo bila kuzingatia imani zao huku jeshi la polisi likisimamia ufuatiliaji wake.

Hadi sasa inakadiriwa kuwa kuna wakristo zaidi ya Milioni 1.5 nchini humo ambao ni wahamiaji wanaofanya kazi hususani kutoka nchi ya Ufilipino.

Uwezekano wa kufanikiwa kwa harakati hizi za Vatican zilizoanza mwaka 2018 ulianza kuonekana baada ya Mwanamfalme Mohamed bin Salman kuingia madarakani ambapo amedhamiria kubadili mambo kadhaa.

Katika kipindi chake tayari ameshabadili taratibu kadhaa zilizokuwepo kwa miaka mingi kama wanawake kutoruhusiwa kuendesha magari na kutakiwa kuwa na mwangalizi muda wote.

 

Mbowe awazungumzia madiwani 46 waliohama Chadema
Kocha wa zamani wa Yanga afariki dunia