Serikali ya Saudi Arabia imezuia wageni wote wanaoingia nchini humo kwa safari za kidini, ikiwemo wanaotembelea miji mitakatifu katika dini ya Kiislamu – Makka na Madina kufuatia mlimpuko wa Virusi vya Corona.

Mamilioni ya watu huingia Saudia mwaka mzima kufanya ibada ya Umra, na wengi zaidi huingia kwa pamoja kufanya ibada ya Hija,ambapo tofauti na Hija, Umra hufanyika katika kipindi chochote cha mwaka, na kwa sasa marufuku hiyo inawalenga mahujaji raia wa nchi za nje wanaoenda kuitekeleza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC bado haijulikani kama ibada ya Hija, ambayo inategemewa kuanza mwishoni mwa mwezi Julai kama itaathirika na zuio hilo.

Wizara ya mambo ya nje ya Saudia imesema marufuku hiyo ni ya muda lakini wizara hiyo haijataja lini marufuku hiyo itaondolewa mpaka sasa Saudia bado haina mtu ambaye amethibitika kuambukizwa virusi hivyo.

Shirika la Afya Duniani (WHO) mapema wiki hii limeonya kuwa dunia inapaswa kujiandaa kwa uwezekano wa janga la virusi vya corona.

Aidha shirika hilo limesema kuwa ni mapema sana kuuita mlipuko wa virusi hivyo janga lakini nchi zinapaswa kuwa katika “awamu ya maandalizi”.

Hata hivyo barani Ulaya hali ni mbaya zaidi nchini Italia ambapo mpaka sasa watu 400 wamethibitika kuambukizwa ugonjwa huo kutoka watu 80 siku ya Jumanne. Watu 12 tayari wameshafariki nchini humo kutokana na mlipuko huo.

Kwa Afrika ni nchi mbili mpaka sasa zimethibitisha kuingia kwa ugonjwa huo. Algeria na Misri kila moja imeripoti mgonjwa mmoja.

Nzige wavamia DRC
Serikali yatoa miezi sita wakopeshaji kushusha riba