Baada ya adha waliyoipata Mahujaji mwaka jana na kupelekea hatua inafuatia mkanyagano  ambapo zaidi ya mahujaji 750 wanaaminikia kufariki  huku wengine 900 wakijeruhiwa Saudia imeweka mikakati kukabiliana na changamoto hizo.

Saudia inatarajiwa kuwapatia bangili za kielektroniki mahujaji wanaoelekea Mecca kwa ajili ya Hijja ya mwaka huu ambalo ni kongomano kubwa la Waislamu kutoka pande zote za  dunia.

picha

Bangili hizo zitakuwa na habari binafsi za kila hujaji pamoja na zile za matibabu kusaidia mamlaka ya Saudia kuwatambua na kuwalinda mahujaji hao.

Aidha Takriban kamera 1000 pia zimewekwa kwa ajili ya ulinzi wakati wa hijja.

Bangili hiyo ya utambulisho itakuwa na habari muhimu kama vile pasipoti na anwani lakini pia zitatoa habari kwa mahujaji kama vile muda wa ibada pamoja na lugha tofauti kuwasaidia wale wasiofahamu lugha ya Kiarabu wakati huo.

Bangili hizo zitakuwa haziingii maji na zitaunganishwa na programu ya ramani

BBC

Video: Ajali mbaya iliyohusisha magari 3 Morogoro
Video: RC Makonda amepokea msaada mwingine Hospitali za Dar es salaam