Tuzo za MTV MAMA zimetolewa usiku wa kuamkia leo jijini Johannesburg, Afika Kusini huku Tanzania ikishindwa kuchomoza na tuzo kwenye vipengele kadhaa ambavyo wasanii wake walitajwa.
Kundi la Sauti Sol la Kenya, limeitoa kimasomaso Afrika Mashariki baada ya kushinda tuzo ya kundi bora la Muziki (Best Group) ambayo ni tuzo pekee iliyokuja katika ukanda huu.
Usiku huo ulikuwa mkubwa zaidi kwa Wizkid ambaye aliibuka na tuzo mbili nzito zaidi, Msanii wa Mwaka (Artist of the Year) na Msanii Bora wa Kiume (Best Male Artist), pamoja na tuzo moja ya wimbo bora wa kushirikiana (DJ Maphorisa Feat Wizkid & Dj Buckz – Soweto Baby). Hivyo kuongoza kwa kuondoka na tuzo tatu usiku huo.
Wasanii wa Tanzania waliotajwa kuwania tuzo hizo ni pamoja na Diamond Platinumz, Ali Kiba, Raymond, kundi la Yamoto Band, Vanessa Mdee na kundi la Navy Kenzo.
Hii ni orodha kamili ya washindi wa tuzo hizo:
Best Live Act: Cassper Nyovest
Best Group: Sauti Sol
Best Pop/Altenative Act: Shekhinah & Kyle Deutsch
Best Female: Yemi Alade
Best International Act: Drake
Best Lusophone Act: C4Pedro (Angola)
Best Francophone: Serge
Best Male: Wizkid
Listeners Choice Awards: Jah Prayzah
Best Collaboration: DJ Maphorisa Feat Wizkid & Dj Buckz – Soweto Baby
Video of the Year – Nique Ma VieYoussoupha (Congo)
Best Hip Hop: Emtee
Breakthrough Act: Tekno
Song of the Year – My Woman (Patoranking)
Artist of the Year – Wizkid