Waangalizi wa anga duniani wamengundua kuwa kuna sayari nne ambazo zimejipanga kwa pamoja na zinatarajiwa kuonekana siku ya Jumapili asubuhi katika anga ya alfajiri.

Kulingana na mtandao wa NBC, Waangalizi hao wamesema kuwa kuanzia alfajiri ya Jumapili wafuatiliaji wa nyota wataona sayari ya Mars’, Venus’, Jupiter, na Saturn zikiwa kwenye mstari mmoja zikitokea kabla jua halijachomoza jambo ambalo wamesema ni la nadra kutokea watu kuona sayari zote hizo kwa pamoja kwa jicho la kawaida bila kutumia kifaa maalumu.

Wataalamu hao wameendelea kusema kuwa ili mtu aweze kuona sayari zote hizo aliye kaskazini anatakiwa kutoka nje saa moja kabla hazijatokeza na kuangaza macho Yake upande ambao jua linachomoza.

Kulingana na shirika la NASA linaliojihusisha na masuala ya anga, sayari zote zitaonekana kwa uwazi kama hakutakuwa na mawingu na anga ikiwa nyeupe na hakutakuwa na haja ya kutumia darubini.

Kwa wanaoishi upande wa kusini wamesema mshale huo wa sayari utatokea juu kidogo ya kuchomoza kwa jua kwa kuwa eneo hilo lipo kwenye kona ya Dunia lakini kwa maeneo yote Jupiter itakuwa sayari ya pili kwa uangavu lakini itaonekana kwa udogo hali itakayofanya kuwa na ugumu wa kuiona na kadri mwezi unavyoondoka ndivyo na sayar hizo zitapotea.

“Kuelekea wiki ya mwisho ya mwezi Aprili sayari ya Jupiter itakuwa angavu zaidi juu ya Dunia na masaa mengi kabla ya kuchomoza kwa jua na kuifanya ionekane kwa urahisi,” wamesema wataalamu wa NASA.

Kulingana na Mtandao wa NBC wataalamu hao wanasema mzima wa April safari hizo zitaonekana na itakapofika mweiz wa June na Julai zitaonekana sayari tano ambazo ni Mercury, Venus, Mars, Jupiter, na Saturn na sitakaa kwa muda angani jambo embalo ni nadra kutokea kwa miaka kadhaa.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, April 17, 2022
Sh. Milioni 215 zaliwa na wafanyakazi 3 MSD