Klabu ya Schalke 04, imekanusha taarifa za mshambuliaji Leroy Sane kufanyiwa vipimo vya afya huko mjini Manchester nchini England, kama sehemu ya uhamisho wake ambao unaendelea kuwa gumzo siku hadi siku.

Sane, yupo kwenye rada za meneja wa Man City Pep Guardiola, na tayari imeripotiwa uongozi wa klabu hiyo ya Etihad Stadium umeshatenga zaidi ya Pauni milion 45 kwa ajili ya usajili wa mshambuliaji huyo wa pembeni.

Gazeti la Kicker quote, limetoa taarifa za fununu za kuondoka kwa Sane ambazo zilienda mbali zaidi kwa kuihusisha safari yake hadi mjini Manchester ambapo iliripotiwa tayari ameshafanyiwa vipimo vya afya.

Mkurugenzi wa michezo wa Schalke 04, Christian Heidel amenukuliwa na gazeti hilo akikanusha taarifa za kuondoka kwa Sane, na amesisitiza jambo hilo kutokua katika hali nzuri kutokana na taarifa zinazoendelea kuzushwa na baadhi ya vyombo vya habari.

“Hakuna ukweli wa jambo hilo na sijui taarifa hizi nani amezieneza katika vyombo vya habari,”

“Hakuna makubaliano yaliyofikiwa kati yetu na Man City, hivi ninavyozungumza Sane, yupo katika kambi yetu nchini Austria kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi, na ataendelea kuwepo hapa.” Alisema Christian Heidel.

Rooney: Sina Muda Zaidi Kwenye Timu Ya Taifa
Senol Gunes Kukwamisha Usajili Wa Mario Balotelli