Aliyekua kiungo wa Man Utd Paul Scholes ameonyesha wasi wasi na kiwango cha kikosi cha klabu hiyo, kwa kusema bado kina kazi kubwa ya kufanya ili kutimiza lengo la kupambana kwenye michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Scholes alionyesha dukuduku lake mara baada ya mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo ambapo ulimwengu mzima ulishuhudia Man utd wakikubalia kupoteza mchezo wa ufunguzi wa hatua ya makundi kwa kufungwa mabao amwili kwa moja dhidi ya mabingwa wa soka nchini Uholanzi.

Scholes amesema kama Man utd wataendelea kucheza kama walivyocheza usiku wa kuamikia hii leo, watakua na shughuli nzito ya kufikia malngo waliyojiweka n ahata ikitokea wanafika katika hatua ya mtoano itakua ni baharti kwao.

Scholes, ambaye anaendelea kukumbukwa kwa mchango mkubwa alioutoa wakati akiitumikia Man utd pamoja na timu ya taifa lake la England, alikua sehemu ya kikosi cha Sir Alex Ferguson kilichotwaa ubingwa wa barani ulaya mara mbili.

Xavi: Guardiola Alinibania Kwenda Bayern Munich
Mourinho: Sikuizoea Hali Hii