Nyota wa Hollywood kutoka nchini Marekani, Arnold Schwarzenegger amesema kuwa hatomfungulia mashtaka mtu aliyemshambulia katika hafla moja nchini Afrika Kusini.

Muigizaji huyo maarufu mwenye umri wa miaka 71 alikuwa akizungumza na mashabiki katika hafla yake ya Arnold Classic Africa Sporting Event siku ya Jumamosi wakati mtu alipomrukia na kumpiga teke mgongoni.

Mshambuliaji huyo baadaye alikamatwa, huku Schwarzenegger akisema kwamba hatomchukulia hatua mtu aliyemshambulia akisema tukio hilo limepitwa na wakati.

Aidha, kanda hiyo ya video ,iliyosamabazwa katika mitandao ya kijamii ilimuonyesha Schwarzenegger akipiga picha na mashabiki wake wakati mtu aliyemshambulia alipotoka nyuma na kupiga flying kick.

Hata hivyo, Schwarzenegger alituma ujumbe wa Twitter kwa zaidi ya mashabiki wake akisema ‘Nilihisi kama kuna mtu kanisukuma kulingana na watu waliokuwa wamejaa katika hafla hiyo, kitu ambacho ni kitu cha kawaida,”ameandika Schwarzenegger

Hafla hiyo ya michezo ya Arnold Classic Afrika hufanyika kila mwezi Mei na hushirikisha michezo kadhaa ikiwemo utunishaji Misuli na michezo ya ngumi.

Mtaelewa tu fitina anazofanya Masele- Spika Ndugai
Makala: Urafiki, uadui wa Osama Bin Laden na Marekani; Al-Qaeda na 'ushetani'

Comments

comments