Mahakama ya Wilaya ya Ilala leo imemfutia mashtaka Salum Njwete maarufu kama Scorpion na kufunguliwa upya mashtaka kutokana na maombi yaliyowasilishwa kwa nyakati tofauti na upande wa Jamhuri.

Mahakama hiyo ilimfutia mashtaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha na baadae kumfungulia mashtaka yanayofanana na hayo kwa mujibu wa sheria inayompa Mamlaka Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri (DPP) kufuta mashtaka aliyoyawasilisha mahakamani lakini pia kufungua mashtaka upya kwa kesi husika kama haijatolewa hukumu.

Akieleza kukubaliana na ombi la DPP, Hakimu Adelf Sachore alikitaja kifungu namba 91, kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya makosa ya jinai kinachotoa nafasi hiyo.

Mshtakiwa huyo ambaye anatajwa na mlalamikaji Said Ally kuwa ndiye aliyebomoa macho, anakabiliwa na kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Hata hivyo, alikana mashtaka hayo na kurudishwa rumande baada ya ombi lake la dhamana kuzuiwa.

Mkuu wa Mkoa Arusha atoa ujumbe mzito baada ya kuzushiwa ‘ametumbuliwa’
Waziri Mkuu amsimamisha kazi Mkurugenzi wa LUWASA